Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yawatahadharisha wananchi na matapeli wanaolipisha kodi mkononi

82357 Trapic TRA yawatahadharisha wananchi na matapeli wanaolipisha kodi mkononi

Thu, 31 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara kutolipa malipo yoyote ya kodi kwa kutoa fedha mkononi, ili kuepuka kutapeliwa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano 30, Oktoba, 2019 na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  juu ya kipande cha picha mjengeo (video) inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mtu aliyekamatwa akikusanya kodi kwa kivuli cha mamlaka hiyo.

“Mtu huyu, inasemekana ni mkazi wa Toangoma jijini Dar es Salaam, aliyejulikana kwa jina la Hassan Mrugulu ametapeli wafanya biashara wa wilaya ya Temeke kwa kujifanya ni mtumishi wa TRA,” amedai kayombo.

Kayombo mtu huyo ambaye anatumia  kitambulisho bandia, amekuwa akitapeli wafanyabiashara na kupokea fedha  mkononi, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa mamlaka hiyo.

“Kwanza ieleweke kwamba mtu huyu si mfanyakazi kabisa wa TRA na hakuna afisa wetu anaye kusanya kodi kwa kuchukua pesa mkononi. Tozo zote hulipwa kwa njia ya benki na simu tu,” alisema.

Laiti waliotapeliwa wangekuwa wanajua utaratibu huu basi ingekuwa rahisi kumnasa mtu yule kabla hajaleta madhara yoyote. “Hata hivyo uchunguzi utafanyika ili kubaini alipata vipi hicho kitambulisho bandia na wapi vinatengenezwa. Pia kufahamu zaidi kama kuna watu anaofanya nao kazi hizo za utapeli,” aliongeza.

Lakini pia TRA imewaomba watu waliotapeliwa na bwana Mrugulu waweze kujitokeza kwenye tawi lake la Temeke na kujiandikisha ili kufahamu idadi ya watu na kiasi cha pesa alizotapeli.

Kayombo alikiri kuwa tukio hilo sio mara ya kwanza kutokea au kuripotiwa, lakini wengi wameshindwa kukamatwa kwa kuwa taarifa zimekuwa zikitolewa kwa kuchelewa.

“Matukio kama haya na yale ya kupigiwa simu wafanyabiashara wakiombwa pesa kwa kutishiwa kufanyiwa mahesabu ya biashara zao yamekuwa yakiripotiwa mara nyingi sana laikini walalamikaji hutoa taarifa kwa kuchelewa sana na wahusika wanakuwa wameshakimbia,” alisema.

Hata hivyo Kayombo alisema kuwa hana takwimu sahihi ya matukio hayo lakini yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma.

Chanzo: mwananchi.co.tz