Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yawapa somo wafanyabiashara kuhusu utunzaji kumbukumbu

Tra Kodi.jpeg TRA yawapa somo wafanyabiashara kuhusu utunzaji kumbukumbu

Sun, 26 Jun 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwa wazalendo kuhakikisha wanajenga utamaduni wa kutunza kumbukumbu ili kulipa kodi sahihi na kwa hiari bila kushurutishwa.

Meneja msaidizi wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Tilson Kabuje ametoa rai hiyo mjini Moshi wakati wa kikao na wafanyabiashara wa spea za magari na pikipiki, vilainishi pamoja na wale wa gereji  kilichokuwa na lengo la kutoa elimu na kusikiliza kero zinazowakabili.

Kabuje amesema ni muhimu wafanyabiashara wakatunza kumbukumbu ili kulipa kodi sahihi na kwa wakati, hatua ambayo itaondoa malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wafanyabiashara, wakidai kutozwa kodi kubwa.

"Ni muhimu wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara zenu na mfanyabiashara hawezi kulalamika kodi kubwa kama anatunza kumbukumbu za biashara yake, niombe tushirikiane ikuhakikisha kila mmoja analipa kodi sahihi na kwa wakati," amesema Kabuje.

Ofisa elimu na huduma kwa mlipa kodi TRA mkoani Kilimanjaro, Odupoi Papa amesema ni haki ya wafanyabiashara kusikilizwa na kuwataka kutoa taarifa pindi kunapotokea changamoto ikiwemo biashara kuyumba.

"Wajibu mmoja wapo kwa mfanyabiashara ni kutunza kumbukumbu za manunuzi na mauzo, lakini pia anayo haki ya kusikilizwa, na inapotokea biashara inayumba, anapaswa kutoa taarifa TRA, tunaomba kila mmoja atimize wajibu wake ili kupata haki"amesema Papa.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa wa Kilimanjaro,  Hilary Lyatuu amesema wafanyabiashara wanapaswa kufahamu haki na wajibu wao ili  kulipa kodi kwa wakati  na kwa hiari bila kushurutishwa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz