Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yawanoa wachimbaji kodi mpya ya asilimia 2

Mkoa Wa Geita Sadick Rutenge TRA yawanoa wachimbaji kodi mpya ya asilimia 2

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Mkoa wa Geita imewatoa hofu wachimbaji wadogo juu ya kodi ya asilimia mbili (2%) ya mauzo itakayoanza kutozwa kwani mabadiliko yamezingatia maoni ya kamati za wachimbaji.

Akizungunzia Kodi hiyo baada ya semina fupi iliyojumuisha mashirikisho ya wachimbaji wadogo ,Madalali, wafanyabiashara iliyofanyika Mjini Geita Ofisa Kodi kutoka TRA Mkoa wa Geita Sadick Rutenge amesema mabadiliko ya sheria yanayofanywa na serikali katika sekta ya madini yanalenga kuongeza tija kwa kupunguza utitiri wa tozo na kuwatia motisha wachimbaji kulipa kodi hivo wayapokee.

“Nia na makusudi ya sheria hii, tuliweza kugundua kwamba kuna wachimbaji wengi ambao wanafanya biashara ya madini ambao kimsingi inakuwa ni ngumu kutunza kumbukumbu zao za uchimbaji.

“Kwa hiyo sheria hii imekuja kwa lengo la kuweza kumfanya mchimbaji mdogo atakapokuwa ameuza madini yake aweze kulipia hiyo asilimia mbili.” Amesema Rutenge

“Sheria hii inawahusu wachimbaji wote ambao wanazalisha dhahabu kwa kutumia leseni ya awali (Primary Mining Licence) pamoja na wale ambao hawana leseni za uchimbaji (artisanal mining)

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wachimbaji wadogo mkoani Geita (GEREMA), Golden Hainga aliiomba TRA kuendelea kutoa elimu ya sheria hiyo mpya ili kuwajengea utamaduni wachimbaji kulipa kodi bila shinikizo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Wanawake mkoani Geita (GEWOMA), Asia Masimba ameiomba serikali kuendelea kuitikia punguzo la kodi kwenye biashara ya madini ili wajiendeshe kwa faida.

Huku baadhi wa wachimbaji wadogo wakiimba Mamlaka ya mapato TRA Mkoa wa Geita kuwa na utamaduni wa kutoa Elimu na mafunzo kuhusu Kodi mpya mbalimbali Ili kuondoa sitonfahamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live