Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yavunja rekodi, yakusanya Trilioni 2.51

IMG 2741 660x400 TRA yavunja rekodi, yakusanya Trilioni 2.51

Sun, 2 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema katika kipindi cha mwezi mmoja tu wa December 2021 imekusanya TZS trilioni 2.51 kati ya lengo la kukusanya Tsh. Trilioni 2.29 ambapo makusanyo haya yamefikia ufanisi wa asilimia 109 na ndicho kiwango cha juu kukusanywa kwa mwezi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mwaka 1996.

Katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2021/22 ambacho ni kuanzia July mpaka Desemba 2021, TRA imekusanya TSh. Trilioni 11.11 kiwango cha pesa ambacho ni sawa asilimia 98 ya lengo la makusanyo ya Tsh. Trilioni 11.302.

Katika taarifa yake, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata amesema “kwa namna ya pekee Mamlaka inapenda kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa miongozo aliyoitoa kwa Mamlaka kutoa huduma zinazozingatia uadilifu, weledi na uwajibikaji ili kukidhi matarajio ya walipa kodi na Wananchi kwa ujumla kwa kuwapatia walipa kodi mazingira mazuri ya kuzalisha mali na rahisi ya ulipaji kodi”

Ameongeza kwamba katika kipindi cha nusu mwaka mwenendo wa ulipaji kodi kwa hiari na uhusiano baina ya Mamlaka na Walipa kodi umeimarika kwa kiwango cha kuridhisha ambapo Mamlaka inapenda kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa Walipa kodi wote na Wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa dhati katika kuwezesha kufikiwa kwa kiwango hiki cha makusanyo hivyo kuiwezesha TRA kuweka rekodi mpya ya ukusanyaji mapato Nchini tangu kuanzishwa kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live