Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yatoa onyo kwa wanaokwepa kulipa kodi

Tax Tax Ushuruuuu TRA yatoa onyo kwa wanaokwepa kulipa kodi

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imetangaza mikakati thabiti kuhakikisha inakabiliana na wafanyabiashara wanaokwepa kodi ili kukomesha tabia hiyo na kuweka usawa katika sekta ya biashara.

Kamishina Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara mjini Geita lengo likiwa ni kupokea malalamiko, ushauri na kujibu hoja za wafanyabiashara.

Mwenda amesema wafanyabiashara wanaofanya urasimu huo siyo tu wanaikosesha nchi mapato bali pia wanarudisha nyuma mipango ya serikali na hivo wanapobainika ni lazima wachukuliwe hatua stahiki.

“Hizi hela siyo za TRA, hizi hela ni za watanzania, TRA wakikusanya wala hawachukui wao, bali zinaenda kwenye mfuko mkuu kwa ajili ya maendeleo, alisema na kuongeza;

“Tunaenda kuimarisha kupata taarifa za wakwepa kodi, tutaimarisha sana vitengo vya uchunguzi na ukaguzi, ili tuwabaini na tukiwabaini tutachukua hatua kali.

"Yani huyu alipe mwingine asilipe harafu mpo kwenye soko moja, hiyo siyo sawa, kwa hiyo tutakwenda kusimamia hilo na msiwatetee wakwepa kodi," amesema Mwenda.

Amesema TRA imejidhatiti kuweka mazingira rafiki ili biashara ziendelee kuanzishwa, kufanyika na kukua zaidi kwani mbali na kuchangia mapato lakini biashara inatoa ajira na huduma kwa watanzania wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live