Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yatoa elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi

Tra Website TRA yatoa elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Katavi imetoa elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Mpimbwe ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumzia utoaji wa elimu hiyo Meneja wa TRA Mkoa wa Katavi, Jacob Mtemang'ombe amesema wamepunguza changamoto nyingi zilizokua zikiwakabili wafanyabiashara wa halmashauri hiyo.

Mtemang'ombe amesema katika mafunzo hayo wamebaini kuna wafanyabiashara wanafanya makosa kwa kuituhumu TRA na serikali kutokana na elimu ndogo ya masuala ya kodi kwabaadhi ya wafanyabiashara hivyo kupitia elimu hiyo wametambua wajibu wao kwamaslahi mapana ya mkoa na nnchi kwa ujumla.

Aidha Mtemang'ombe amesema matarajio yao ni kuona muamko mkubwa wa utii wa sheria bila shuruti ikiwemo watu kutumia mashine za kielektroniki kwakutoa risiti kwa usahihi na kudai risiti pale wanapofanya manunuzi.

Wakati wakitoa kero zao wafanyabiashara hao wamewaomba maafisa wa TRA kutotumia madodoso pekee kumkadiria mfanyabiashara kodi anayotakiwa kulipa badala yake wafike eneo la biashara kujionea hali halisi ya biashara inayofanyika ili kodi inayolipwa iendane na uhalisia wa biashara ya mtu.

Aidha wafanyabiashara hao wamewashukuru maafisa wa TRA kwa kuona umuhimu wa kuwapa elimu ya kodi na kuwakumbusha kulipa Kodi kwa njia ya simu huku wakidai kufanya hivyo kunawasaidia kuepuka faini lizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live