Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yataka wageni kufuata taratibu Kigoma

56724 Pic+tra

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara wanaotoka nchi jirani wanaotaka  kuwekeza mkoani Kigoma kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na kuacha kutumia njia zisizo rasmi.

Rai hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 10 na mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo katika kongamano la biashara la nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika.

Aliwataka wafanyabiashara wajitokeze kufanya biashara mkoani humo na kufuata maelezo sahihi kwani kodi wanayotozwa ni rafiki.

Amesema endapo watazingatia taratibu wataelekezwa nini cha kufanya kutokana na biashara wanayotaka kuanzisha mkoani humo na kuacha kutumia watu ambao sio watumishi wa Serikali.

"Wafanyabiashara wanaotoka nchi za jirani na kutaka kuwekeza mkoani Kigoma waache kutumia watu ambao si rasmi wanaweza kutapeliwa na kukosa msaada, mara nyingi watu wanapata matatizo kwa sababu ya kutofuata maelezo sahihi, " amesema Kayombo.

Kayombo amesema kuanzia Mei 13 hadi 17 mwaka huu   TRA itatoa elimu ya huduma kwa wafanyabiashara wote nchi nzima kwa lengo la kujua changamoto wanazokabiliana nazo na kuwatembelea mmoja baada ya mwingine katika maeneo yao ya biashara.

Meneja wa Mamlaka ya Bandari mkoani Kigoma, Ajuaye Msese amesema tozo zipo kisheria akibainisha kuwa  pamoja na kutoa huduma lakini wanafanya biashara.

Amesema katika ukanda wa ziwa Tanganyika bandari yao ndio yenye gharama nafuu ikilinganishwa na bandari nyingine katika nchi hizo.



Chanzo: mwananchi.co.tz