Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yatahadharisha wafanyabiashara marejesho ya ritani

Bb483d977a66027cd262332abc87a3e9.png TRA yatahadharisha wafanyabiashara marejesho ya ritani

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imewatahadharisha wafanyabiashara kuepuka kufanya udanganyifu katika mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielekroniki unaotegemewa kuanza kutumika mwezi Machi.

Akitoa elimu kwa wafanyabiashara katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Afisa elimu kwa walipa kodi mkoani Kagera amesema serikali inaendelea kuboresha mfumo huo na iko tayari kumuelimisha mfanyabiashara mahala popote na kwa wakati wowote.

“Ni mfumo mpya unaotarajiwa kuanza kutumika mwezi huu,” amesema. Mfumo huo unawataka wafanyabiashara kuepuka kufanya udanganyifu na kanuni zimeweka masharti ya adhabu ya Sh 250,000 kwa kampuni na Sh 75,000 kwa mtu binafsi kwa mwezi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz