Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yasitisha minada ya hadhara, yaanzisha ya kielektroniki

89824 TRA+PIC TRA yasitisha minada ya hadhara, yaanzisha ya kielektroniki

Thu, 26 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesitisha minada ya hadhara ya bidhaa mbalimbali na kuanzisha mfumo mpya wa minada hiyo kwa njia ya kielektroniki.

Mfumo huo utaondoa vitendo vya rushwa na kupanua wigo wa biashara kwa kuwajumuisha wanunuzi kutoka nje ya nchi pamoja na kupunguza mrundikano wa mizigo katika maeneo mbalimbali ikiwamo maghala ya forodha, ofisi za posta, bandari kavu na kituo cha kuondosha mizigo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 24, 2019 jijini Dar es Salaam, Kamishna wa TRA, Dk Edwin Mhede amesema kwa mara ya kwanza mnada huo utafanyika Januari 2, 2019.

“Minada hii ya hadhara ilikuwa ikifanyika kila wiki mara moja na kwa kiasi kikubwa bidhaa zilikuwa haziuzwi kwa wakati na kupelekea Serikali kutokomboa kodi yake kwa wakati huku washiriki wa mnada wamekuwa ni walewale kwa kujirudia rudia,” amesema Dk Mhede

“Kupitia utaratibu wa minada ya forodha kwa bidhaa mbalimbali kwenye maeneo ya forodha umekuwa ukifanywa kupitia dalali aliyepewa kandarasi na TRA kufanya minada hiyo ambayo kwa sasa kila kitu kitakuwa kikiendeshwa kwa njia ya mtandao,” amesema

Amesema mrundikano wa bidhaa ambazo zimeshindwa kulipiwa kodi katika maeneo hayo ulikuwa ukizorotesha utendaji kazi maeneo husika.

“Lakini pia gharama ambazo zilikuwa zikitumika katika kuendesha minada hiyo ni kunwa na hivyo kazi hii kufanywa kwa tija ndogo kuanzia sasa,” amesema Dk Mhede

Chanzo: mwananchi.co.tz