Wakati kampeni ya kukamata watu wasiotoa na wasiodai risti ikitajwa kuanza leo nchi nzima, Serikali imepunguza kigezo muhimu cha wafan-yabiashara wanaotakiwa kuwa na mashine za kielektroniki za kutolea risiti(EFD).
Kigezo kilichokuwepo kuwa na mashine ya EFD ilikuwa ni lazima mauzo ghafi kwa mwaka yawe kuanzia Sh14 milioni ambayo ni takribani Sh40,000 kwa siku, lakini sasa kulingana na tangazo jipya la TRA itakuwa Shll milioni ambayo ni sawa na Sh30,000,hatua hiyo ambayo inatajwa kama njia ya kupanua wigo wa walipa kodi.
"EFD inasaidia kuondoa utata na ubishi kwa kuhakikisha kunaku-wa na utunzaji mzuri wa taarifa za mauzo ya mlipa kodi,lengo si kusumbua wafanyabiashara, bali wawajibike," alisema jana, Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.
Kayombo ambaye alikuwa akizungumzia kampeni ya Kamata wote' inayoendeshwa na TRA nchini kwa ajili ya kuwabaini na kuwachukulia hatua watu wote wasiotoa na kudai risiti,alisema hivi sasa kumekuwa na ukikwaji wa utaratibu wa kisheria kwa makusudi.
"Ili kuhakikisha suala hili linatekelezwa kikamilifu,utaratibu wa kisheria wa kusimamia hilo umeweka ambapo kwa muuzaji anayekiuka utaratibu kuna adhabu ya faini ya Sh3 milioni hadi Sh4.5 milioni au vyote kwa pamoja na kwa mnunuaji ni Sh30,000 hadi Sh1.5 milioni kulingana na thamani ya bidhaa atakayokutwa nayo " alisema.