Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yaonya upotoshaji namba ya mlipakodi

Efdpic Data TRA yaonya upotoshaji namba ya mlipakodi

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) mkoani Geita, imewataka Watanzania hususani wakazi wa Geita kuachana na dhana potofu kwamba Namba ya Mlipakodi (TIN), inatolewa kwa ajili ya watu kulipa kodi peke yake.

Ofisa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA mkoani Geita, Justine Katiti amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.

Amesema watu wamekuwa na maswali kuhusu TIN na kudhani ni kwa ajili ya biashara tu, lakini sheria inaelekeza kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 mwenye namba ya NIDA anapaswa apate TIN-Namba.

Amesema watu wengi wanakuwa wana tafsiri kwamba ukishapata TIN Namba unaanza kulipa kodi, lakini siyo sahihi kwamba ukishapata TIN hapo hapo na kodi ya mapato sio sahihi.

“Inategemea hiyo TIN-namba unaitumia kwa matakwa gani kama ni ya biashara basi utaitumia kulipa kodi, lakini pia unaweza kuitumia kulipa ada na mambo mengine,” amesema.

Amesema pia TRA inaendelea kutoa elimu juu ya makadiro ya kod, ili kuepusha sintofahamu kwa wafanyabiashara, kwani TRA inakadiria kodi kwa kuzingatia mapato na sio mtaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live