Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kigoma imesema kuwa serikali isipokusanya mapato haitaweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi wala kutekeleza miradi ya maendeleo.
Meneja wa mamlaka hiyo mkoani humo, Deogratias Shuma amesema wakati akiongea na wanafunzi pamoja na wanachama wa klabu ya walipa Kodi (Tax clab) ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kigoma Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati akikabidhi misaada ya aina mbalimbali za juice kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Shuma alisema kuwa msingi wa serikali katika kuwahudumia wananchi wake ni kukusanya mapato ya ndani ya kutosha na hata mikopo na misaada kutoka nje inawezesha kusaidia serikali inapoishi ambayo nayo pia inasisitiza ukusanyaji wa maapato ya ndani hivyo wananchi wanalo jukumu kubwa la kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali.