Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yalia na magendo maeneo ya mpakani

Magendo TRA TRA yalia na magendo maeneo ya mpakani

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kutembelea maeneo ya mipakani ikiwa ni hatua ya kutoa elimu kuhusu biashara za magendo kwa bidhaa zinazoingia na kutoka nchini bila kufuata taratibu za kisheria.

Maofisa wa Forodha wa mamlaka hiyo Wamefika katika mpaka wa Namanga na eneo la Mundarara Longido kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wanaozunguka maeneo hayo Mkoani Arusha.

Akitoa Elimu katika eneo hilo, Afisa Msimamizi wa Kodi Julieth Kidemi amezitaja athari za Magendo kuwa nì kuhatarisha afya za watumiaji wa bidhaa zilizoingia bila kupitia maeneo yaliyo ainishwa na Serikali kwa ajili ya ukaguzi na kupimwa kama zinafaa kwa matumizi ya binadamu.

Kufuatia hatari hiyo ametoa rai kwa wananchi katika eneo hilo kutumia mipaka rasmi ambayo imewekwa na Serikali katika uingizaji na utoaji wa mizigo, lengo likiwa ni kuthibitisha ubora wa bidhaa kutoka mamlaka husika.

Kwa upande wake, Meneja Msaidizi wa forodha Mkoa wa Arusha, Paul Kamukulu ameshukuru ujio wa Maafisa kutoka kitengo cha elimu kwenda kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wanaokaa maeneo ya mipakani kuhusiana umuhimu wa kupita mipaka iliyo rasmi, hivyo kwa elimu hiyo itawasaidia wananchi kuacha kuingiza bidhaa za magendo na kufata taratibu zilizowekwa na Serikali.

Nao wafanyabiashara waliopata Semina hiyo wameishukuru TRA, huku wakiomba Serikali kupunguza makali ya sheria za mipakani ili waweze kufanya biashara zao bila vizuizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live