Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yakusanya tril 5.9 Jan-Machi

Fedhaa 0 TRA yakusanya tril 5.9 Jan-Machi

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (“TRA” au “Mamlaka”) imesema katika kipindi cha robo ya tatu (January – March) ya Mwaka wa Fedha 2022/23, imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 5.9 sawa na ufanisi wa asilimia 97.9 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 6.0.

Makusanyo haya ni sawa na ongezeko la asilimia 6.1 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha 2021/22.

Makusanyo haya kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji kodi ambayo imerahisisha utaratibu wa ulipaji kodi kwa hiari, kuongezeka kwa uwezo wa walipakodi katika kulipa malimbikizo ya kodi kutokana na Serikali kuongeza kasi ya kulipa marejesho ya kodi (tax refunds).

Sababu nyingine ni kuimarika kwa mahusiano baina ya Mamlaka na walipakodi ikiwemo utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya mahakama pamoja na kushughulikia malalamiko ya walipakodi kwa wakati na kujengeka kwa imani kwa Wafanyabiashara kufuatia uwezeshaji wa mazingira mazuri ya biashara nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live