Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yakusanya Tsh trilioni 22.28 2021/22

Efdpic Data TRA yakusanya Tsh trilioni 22.28 2021/22

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kiasi cha Sh22.28trilioni kati ya Julai 2021 hadi Juni 2022, sawa na ufanisi wa asilimia 99.22 ya lengo la makusanyo ya Sh22.45trilioni.

Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la Sh4.13trilioni ikilinganishwa na kiwango cha makusanyo ya Sh18.15trilioni kilichofikiwa kwa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2020/21. Ongezeko hilo ni sawa na ukuaji wa makusanyo kwa asilimia 22.77.

Kwa mujibu wa taarifa ya TRA iliyotolewa leo Julai 3, mwaka 2022 inaeleza katika robo ya nne ya 2021/22, makusanyo yalikuwa Sh5.59trilioni kati ya lengo la makusanyo ya Sh5.3trilioni, sawa na ufanisi wa asilimia 105.47.

“Ufanisi huu wa kiutendaji ni matokeo ya kuendelea na matumizi ya mifumo ya kieletroniki katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi, mazingira ya ufanyaji biashara nchini na mwenendo wa ulipaji kodi kwa hiyari,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live