Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yakusanya Sh12 bilioni kutoka Google

FEDHA WEB TRA yakusanya Sh12 bilioni kutoka Google

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya kodi ya Sh12 bilioni kutoka kampuni zinazofanya kazi Tanzania lakini hazina ukaazi nchini humo ikiwamo kampuni ya Marekani ya Google LLC.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Hudson Kamoga alipozungumza na Mwananchi Digital, muda mfupi baada ya kuwasilisha mada katika mkutano mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaohudhuriwa na wanachama zaidi ya 150.

Kamoga amesema kodi hiyo imekusanywa baada ya kupitishwa kwa sheria ya Fedha ya mwaka 2023 hadi kufikia Machi 2024, na akazitaja kampuni zingine za mtandaoni ambazo kwa mujibu wa sheria hiyo zinapaswa kulipa kodi hiyo na zimeanza kulipa kuwa ni Tiktok, Facebook na Netflix.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live