Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yaeleza faida za mashine za ETS

Mashine ETS TRA yaeleza faida za mashine za ETS

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wazalishaji, wafanyabiashara na kampuni za kanda ya ziwa kuzingatia utoaji wa risti za kieretroniki maarufu kama ETS kwani zinaleta faida kwa Serikali na kwa kampuni kwa ujumla.

Haya yamebainishwa na Kamishina Mkuu wa TRA Alphayo Kidata, wakati alipotembelea kiwanda cha bia cha Seregenti Breweries Limite SBL na kuongeza kuwa mfumo huo sio tu kwamba unasadia kutambua idadi ya mauzo peke bali unaisaidia pia Serikali kutambua kasi ya uzalishaji wa viwanda husika.

"Hii inatusaidia kujua kiasi cha mapato kinachokusanywa na wazalishaji na kitasaidia Serikali kupanga matumizi" Amesema Kidata.

Mfumo huu unawasaidia TRA na wazalishaji wote kwa ujumla kuweza kutambua kiasi cha mapato na kuzuia hasara zinazoweza kujitokeza pamoja na wizi wa maeneo ya kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live