Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yabisha hodi kodi za mtandaoni

Social Media.png TRA yabisha hodi kodi za mtandaoni

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza majadiliano na Kampuni ya Meta inayomiliki mitandao ya Facebookapp, Instagram na Twitter kwa lengo la kuanza kukusanya kodi katika kidijitali kupitia huduma zake nchini.

TRA jana Alhamisi Aprili 21, 2022 ilitoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter ikieleza kufanya mazungumzo hayo jijini Dar es Salaam.

“Timu ya wataalamu wa Kampuni ya @meta inayomiliki mitandao ya @facebookapp @instagram pamoja na @whatsApp leo 21 Aprili, 2022 imefanya mazungumzo ya awali na TRA kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma zao nchini,” imeandika katika ukurasa huo wa TRA.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alipoulizwa alisema mazungumzo hayo yanalenga mpango wa Serikali kuanza ukusanyaji wa kodi katika huduma wanazofanya wamiliki wa mitandao hiyo hapa nchini.

“Kwa ujumla, mazungumzo haya tumeangalia uzoefu wa mataifa mengine yaliyofanikiwa kuanza ukusanyaji wa kodi kupitia huduma za aina hii,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live