Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA watoa ufafanuzi wa kina kuhusu watumiaji wa WhatsApp, Instagram, Facebook kulipa kodi,

Makosa Mtandao kumeibuka maswali ambayo yalikosa majibu kuhusu tozo ya mitandao tajwa

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kwa Mkurugenzi wake wa huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo imetoa ufafanuzi baada ya TRA kukutana na Timu ya Wataalam wa Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp ambapo kwa pamoja wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma hizo nchini.

"Mkutano kati ya TRA na kampuni ya META ulikuwa ni mkutano wa awali wao kuweza kuelewa mazingira ya sheria za kodi za Tanzania na pia kuweza kutupitisha katika jinsi wanavyofanya biashara yao na wanavyotozwa kodi katika Nchi nyingine.

"Lengo ni kufikia mahali huko mbeleni ili kampuni hiyo ichangie kodi kwa pesa inayopata kutokana na biashara inayofanyika hapa nchini kupitia mitandao, Wananchi hawatakiwi kuwa na hofu yoyote kwasababu hii inahusu biashara inayofanyika na kampuni hiyo katika Nchi mbalimbali.

"Na hili sio jambo geni lipo dunia nzima, tumesikia Kenya tayari hilo lipo, Benin, Cameroon na Nchi za Ulaya ambako kampuni hizo kubwa za mitandao duniani zinachangia kodi kwa kufuata sheria za nchi husika na taratibu za kimataifa," - Kayombo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live