Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA watoa stika zoezi kuhamasisha utoaji risiti

TRA TRA watoa stika zoezi kuhamasisha utoaji risiti

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, Mkoa wa Kikodi wa Kariakoo imebandika stika maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti pale wanapouza bidhaa zao na wananchi kudai risiti, ambayo itakuwa thamani sawa na bidhaa waliyonunua kwa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga amesema kuwa kampeni hiyo itakuwa maalumu kwaajili ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mashine za kieletroniki – EFD, kwa wafanyabiashara nchini.

Amesema, “unapouza toa risiti na vile vile unaponunua bidhaa udai risiti yako. Tumebaini kuporomoka kwa utoaji wa risiti kwa sababu risiti zinazotolewa zimekuwa tofauti na matarajio nayo inapelekea makusanyo kushuka.”

Beyanga amefafanua faida za kutoa na kudai risiti pale biashara inapofanyika kuwa inasaidia kutunza kumbukumbu katika ukadiliaji wa mapato yanayoendana na uhalisia wa biashara ambayo mfanyabiashara amefanya pamoja na kuchangia pato la taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live