Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA na usajili wa walipa kodi wapya milioni mbili

00a4a244a48397213abc9f29d75a3a71 Mamalaka ya Mapato Tanzania

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejipanga kusajili walipakodi wapya milioni mbili katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 kupitia kampeni yake ya kusajili walipokodi wapya iliyoanza katika mkoa wa Dar es Salaam tangu Agosti 2, mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa sasa kuna jumla ya walipokodi milioni 3.8 nchi nzima, hivyo lengo lao ni kuongeza walipokodi wapya milioni mbili kupitia kampeni hiyo.

Aliongeza kusema kuwa kampeni hiyo imeanzia Dar es Salaam kwa kuwa mkoa huo ni kitovu cha biashara na asilimia 60 ya walipakodi nchini wapo mkoani humo.

“Kampeni hii tumeianza katika mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya zake zote na tutaifanya kwa mwezi mzima kuanzia Agosti 2 hadi 31 mwaka huu. Tuna timu katika maeneo mbalimbali, japo tumeanza lakini uzinduzi rasmi utafanywa na Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Kamishna Mkuu wa TRA,”

Alifafanua kuwa kampeni hiyo itawashirikisha Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi watendaji ilikurahisha utendaji wa kampeni hiyo itakayo ruhusu wafanyabiashara kufanya biashara zaom katika mazingira rafiki na tulivu badala ya kukimbia kimbia.

Kayombo alisema kampeni hiyo ya kusajili walipakodi wapya itaenda sambamba na kuangalia matumizi ya mashine za EFD katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha watu wanazitumia pasipo shuruti.

Chanzo: www.habarileo.co.tz