Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA kuja na mfumo wa kisasa usimamizi wa kodi

Tax Tax Ushuruuuu TRA kuja na mfumo wa kisasa usimamizi wa kodi

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata, amesema ili kusaidia serikali kutekeleza ajenda mbalimbali za maendeleo endelevu ni muhimu kwa mamlaka za mapato kuwa na mfumo wa kisasa wa usimamizi wa kodi katika ukusanyaji wa rasilimali za ndani.

Kidata amesema hayo leo katika ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Makamishna wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki, ambao mwaka huu unafanyika jijini Dar es Salaam na kusema kuwa kupitia mkuatano huo makamishna hao wanatarijia kujifunza mambo mbalimbali, ikiwemo upande wa teknolojia kwa nchi zilizofanikiwa kwa ajili ya kuweka usawa katika soko.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk Natu El-maamry Mwamba, amesema mkutano huo utazungumzia mambo ambayo yataleta ufanisi zaidi, ikiwemo mifumo ya ukusanyaji kodi, ambazo ni muhimu ziwe na usawa kutokana uwepo wa ushirikiano wa nchi hizo katika biashara za kuvuka mipaka.

Naye Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Uganda ( URA), John Musinguzi ameipongeza Tanzania kwa kuandaa mkutano huo wa kipekee kwa mamalaka za mapato, ambao hutumika kubadilishana ujuzi kwa nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live