Mamlaka ya mapato Tanzania ((TRA) Mkoa wa Pwani imesema kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto ya wimbi la baadhi ya watu kujihusisha na biashara za magendo hali hali ambayo inasababisha serikali kuikosesha sehemu kubwa ya mapato yake.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi na kuongeza kuwa kumekuwa na pia na udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara kutumia stempu ambazo ni bandia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani ameutaka Uongozi wa TRA kubuni Vyanzo vipya vya Mapato visivyowaumiza walipakodi hali itakayoleta uwiano Mzuri na kuongeza Pato la Taifa.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya biashara viwanda na kilimo (TCCIA) Mkoa wa Pwani ameiomba TRA kuweka mipango ya kutoa elimu kwa mlipa kodi na kugagua hesabu za mlipa kodi kwa kila mwaka ili kubaini makusanyo.
Katika hatua nyingine Naibu Kamishna wa TRA kutoka makao makuu alibainisha kuna baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa kutumia mashine za EFD.
Alibainisha kwamba kuwepo kwa changamoto hiyo kubwa kunachangia upotevu wa mapato ya serikali kutokana na vitendo vya kuingizwa bidhaa kwa njia sizizo halali Alisema biashara ya Magendo ambazo zimekuwa zikipitishwa katika njia hizo zimekuwa zikiingia nchini na kuathiri soko la bidhaa za ndani kushindwa kushindana kutokana na bidhaa hizo kuingia bila kulipiwa Kodi na baadhi kukosa ubora.
“Changamoto kubwa (TRA) tunayokabiliana nayo Kwa Sasa Kwa mkoa wa Pwani ni biashara ya Magendo zambazo zinafanyika Kwa bidhaa kuingizwa nchi kupitia njia za panya ambazo ni nyingi pembezoni mwa Pwani ya Bahari ya Hindi”alisema Aidha alisema kuwa hivi sasa mamlaka hiyo imeboresha utendaji wake wa kazi kutoka ule wa zamani wa kutumia nguvu na sasa wamejikita zaidi kutoa elimu kwa wafanyabiashara hivyo kujenga mahusiano bora kati ya pande zote mbili.