Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA: Kodi ya pango sio mpya

Kodi Pango Tra TRA: Kodi ya pango sio mpya

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu kodi ya pango ikisema kawa sio mpya bali wigo umengezwa kwa wapangishaji wa nyumba binafsi kama ilivyokuwa kwa wenye nyumba za biashara ambapo nao wamejumuishaa kwenye wigo wa kodi kuanzia July Mosi 2022.

Taarifa hiyo iliyotolewa leo Ijumaa Agosti 26, 2022 na Idara ya huduma na Elimu kwa Mlipakodi imesema

“Tunapenda kuwafahamisha Wananchi kuwa kodi hiyo sio mpya bali wigo umeongezwa ili Wapanganishaji wa nyumba binafsi kama ilivyokuwa kwa wenye nyumba za biashara nao wamejumuishaa kwenye wigo wa kodi kuanzia July Mosi 2022”

“Mwenye nyumba atapata cheti cha kodi ya zuio kama ushahidi wa malipo ya kodi iliyolipwa kutokana na zuio la asilimia 10.

Akiwa katika mafunzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022 wilayani Bariadi jana Ofisa huduma na elimu mkuu kutoka TRA, Eugenia Mkumbo aliwasisitiza wapangaji kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live