Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA Iramba wahimizwa kasi ukusanyaji kodi

Adca571fe06e4cd23097f76ed6f9fdc2 TRA Iramba wahimizwa kasi ukusanyaji kodi

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Emmanuel Luhahula ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani humo kuongeza juhudi za ukusanyaji kodi ili kuwezesha miradi inayotekelezwa na serikali ifanikiwe.

Aidha, Luhahula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Kodi, amempongeza Meneja wa TRA wiyalani humo, Novline Munuo kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha ukusanyaji wa kodi unaimarika.

Luhahula aliyasema hayo juzi alipozungumza kwenye kikao kazi cha ushauri wa kodi kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa halmashauri ya wilaya hiyo, mjini Kiomboi. Aliitaka TRA wilayani humo kuongeza juhudi za ukusanyaji kodi kwani miradi mingi inayofanywa na serikali kwa ajili ya huduma mbalimbali inatokana na kodi za wananchi.

Alisema kuwa ongezeko la ulipaji kodi ndio chachu ya ongezeko la shughuli mbalimbali za huduma za maendeleo katika jamii na alisisitiza kuwa kulipa kodi ni alama ya uzalendo na si adhabu.

“Kulipa kodi ni alama ya uzalendo si adhabu, ni mpango wa serikali kuipeleka mbele nchi kimapato na kukuza uchumi wake,” alisema Luhahula.

Naye Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, alisema kuwa kulipa kodi ni mchango wa lazima ambao umewekwa kisheria kwa raia na wageni kwa lengo la kukusanya mapato kwa ajili ya matumizi ya taifa.

Akizungumzia masuala ya makadirio, Waziri Mwigulu aliitaka TRA kuhakikisha wanatenda haki kwa kuangalia uhalisia wa biashara au huduma inayotolewa. “Kwa sababu unaweza kumpa mtu makadirio ya juu badala ya kumsaidia ukidhani kwamba ndio utapata kodi kumbe umechochea kufungwa biashara.

“Mkiwapa kodi ambayo ni halali watajua ni wajibu wao na wataweza lakini niwaambie kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli inawapenda walipa kodi na wafanyabiashara hivyo wahimizwe kuhakikisha wanalipa kodi,” alisema Mwigulu.

Alisema ulipaji wa kodi ndio uti wa mgongo wa taifa lolote hivyo hawana budi kujipanga vizuri kuhakikisha watumishi wa TRA na wafanyabiashara hawajengeani mazingira ya chuki na walipa kodi ambao ni wananchi.

Chanzo: habarileo.co.tz