Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA: Hatujapata tatizo stempu za kielektroniki

65942 TRA+PIC

Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haijapata changamoto zozote kuanzishwa na kutumia mfumo wa stempu za kielektroniki (ETS).

Akizungumza mwanzoni mwa wiki katika maonyesho ya 43 ya biashara ya Sabasaba (DITF), Kamishna mkuu msaidizi wa TRA, Msafiri Ndimbo alisema awamu ya kwanza ilizinduliwa Januari 15 mwaka huu na awamu ya pili ilnasubiri kupitishwa Kamishna mkuu ili ianze kutumika.

Alisema awali ETS inaanzishwa kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wazalishaji kuwa inaongeza gharama za uzalishaji. Hata hivyo, Ndimbo alisema uwekwaji kifaa cha stempu hizo hufanywa na TRA, hivyo gharama za wafanyabiashara ni za stempu tu ambazo pia zitapunguzwa na mfumo wa uzalishaji wa kampuni.

Ndimbo alisema awamu ya pili inasubiriwa kuzinduliwa kwa wazalishaji vinywaji vya kaboni na vinywaji baridi, kwa kuwa wameshaweka vifaa muhimu ikiwamo vya kuchapisha na kuhifadhi kwa kampuni zilizo tayari kuanza.

Taarifa zinaonyesha uwekaji wa vifaa vya stempu hizo umeshaanza katika kampuni ya Sigara na Nyati Spirit za Dar es Salaam, huku stempu zikianza kutumika katika bidhaa kama sigara, vileo na vinywaji visivyo na kileo, dawa, karata, maji ya chupa, vipodozi, leseni za uwindaji, usajili wa silaha za moto na vifaa vya muziki.

Serikali iliipa zabuni kampuni ya SCPA Ltd ya Uswis kuweka mifumo ya stempu hizo. Taarifa zaidi zinaonyesha kuwapo kwa malalamiko ya wazalishaji wa bidhaa kuwa mfumo huo huongeza gharama za uendeshaji.

Pia Soma

Wazalishjaji na waagiozaji wasiotumia mfumo huo waliruhusiwa kutumia stempu za karatasi hadi Septemba 2018, baada ya hapo walipewa miezi mitatu ya kubadilisha mfumo huo.

TRA inategemea mfumo huo utaongeza uwazi katika ukadiriaji kodi kama ushuru wa forodha, kodi ya ongezeko la thamani (Vat) na kodi ya shirika.

Chanzo: mwananchi.co.tz