Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA Geita yavuka lengo la makusanyo

Untitled 1 (1) TRA Geita yavuka lengo la makusanyo

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: EATV

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani Geita Hashim Ngoda amesema wamevuka lengo la makusanyo kwa asilimia 132 katika kipindi cha robo ya kwanza mwaka 2022/2023 ambapo walitakiwa kukusanya shilingi bilioni 8.9 kuanzia Julai mpaka Septemba lakini wamekusanya shilingi bilioni 11.9

Hayo yamesemwa na Meneja wa TRA mkoa wa Geita Hashim Ngoda wakati anatoa taarifa kwa waandishi wa habari na kusema ungezeko hilo limelizidi makusanyo ya mwaka wa fedha ulioisha 2021/2022 kwa 67%.

"Kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha , mkoa wa Geita tulikuwa na lengo la bilioni 8.9,  lengo letu kwa quarter tulikuwa na bilioni 8.9 kwa maana ya Julai mpaka September  ambayo tumetoka kuimaliza hivi ponder mpaka tunamaliza quarter tuneshafikia lengo la makusanyo ya kiasi cha bilioni 11.9 ambayo ni wastani wa ufanisi wa asilimia132 la lengo tulilopangiwa ukifannaisha na kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2021"

"Tuna ongezeko la ukuaji wa mapato kwa asilimia 67 ya lengo tulilopangiwa kukusanya kwa kipindi kama hicho kwahyo Geita tunakwenda vizuri na kwa mwezi tu pekee wa 9 tuliotoka kuumaliza ambao tulikuwa na lengo la kukusanya bilioni 3.1 ambapo hadi mwisho wa mwezi tumekusanya kiasi cha shilingi Bilioni 3.9 ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 124 ya lengo alisema Ngoda.

Aidha Ngoda amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuwa na uelewa juu ya Elimu ya ukipaji kodi iliyopelekea wao kuvuka malengo kwa kipindi cha robo ya kwanza.

"Kwa hiyo tunawashukuru wadau wetu, walipa kodi wote Geita kwa kulipa kodi zao kwa hiari na kuchangia mapato ya serikali, kwahiyo Geita tunakwenda vizuri kwa upande wa makusanyo, changamoto zilizokuwepo ni za kawaida tunaendelea kuzitatua, tunapenda kuwaimiza walipa kodi wetu waendelee kutoa risiti kadri qanavyouza na wananchi  kudai risiti kadri wanavyonunua", alisema Ngoda.

Chanzo: EATV