Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPSF kuainisha fursa zilizopo kwenye mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji

59556 Tpsfpic

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta binafsi  Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Baraza la taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Mamlaka ya udhibiti wa nishati, maji na mafuta (Ewura) watawakutansiha wadau kujadili fursa zilizopo kwenye mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mei 24, 2019  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye amesema kuwa mkutano huo utafanyika Juni 11, 2019 .

Amesema mkutano huo utaongeza uelewa wa wadau kwenye mradi huo na fursa zilizopo ambapo miongoni mwa watakaohudhuria ni pamoja na wakandarasi kutoka nchini Misri wanaotekeleza mradi huo.

“Pamoja na wakandarasi wa mradi pia, watakuwepo wanaosimamia utekelezaji ambao ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao watatoa mawasilisho kwa wadau waliohudhuria”amesema Simbeye

Amefafanua kuwa mkutano huo pia utawapa fursa wafanyabiashara na wadau nchini kuwasikiliza wakandarasi kutoka Misri juu ya mpango wa wa kushirikisha wazawa katika utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa NEEC Bengi Issa amesema kuwa katika mradi huo wanategemea ushiriki wa Watanzania katika maeneo yote.

Pia Soma

Amesema mkandarasi atakayetekeleza anapaswa kutoa mpango atatenga ajira kiasi gani kwa  Watanzania, katika ameneo gani na mafunzo ikiwamo kuwafundisha utaalamu.

“Jukumu letu kama Serikali kuwaandaa watu wetu kwa kuhakikisha tuna kanzi data ya watu ambao watafanya kazi pale, na wafanyabiashara ambao wanataka kuingia kwenye mradi huo na jamii inayouzunguka itanufaika vipi, ”alisema Issa.

Chanzo: mwananchi.co.tz