Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPSF, Trademark East Africa wajazwa mamilioni ya kufadhili mikutano

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Trademark East Africa (TMEA) wamesaini mkataba wa makubaliano ya kufadhili mikutano ya kibiashara baina ya sekta binafsi na umma (PPDs).

Mkataba huo utagharimu Sh2.7 bilioni ndani ya miaka mitatu ambapo unatarajiwa kufikia mwisho Juni 2022.

Akizunguza wakati wa utiaji saini leo Jumatatu Juni 3, 2019, mkurugenzi wa Trademark Tanzania, John Ulanga amesema fedha hizo zitasaidia majadiliano ambayo yatajikita katika masuala ya biashara, usafirishaji, saera na sheria mbalimbali ambazo zitarahisisha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji.

"Tanzania ina fursa nyingi sana kibiashara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika mashariki kutokana na Jiografia yake ya kupakana na nchi sita zisizo na bandari, tunaamini fedha hizi zitasaidia mijadala ambayo itaifanya nchi kutumia vema fursa iliyopo," amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema fedha hizo zitatatua changamoto ya uhaba wa fedha uliokuwa kikwazo kikubwa wakati wa kuandaa mijadala.

"Tukiwa na fedha hizi hata tafiti nyingi zitafanyika ili kujua tatizo kiundani kabla ya kupendekeza kwenye mijadala," amesema.

Pia Soma

Simbeye amesema mijadala ya kibiashara katika mikoa na wilaya imekuwa ikishuka mwaka hadi mwaka kutokana na ukosefu wa fedha za tafiti na kuandaa mijadala hiyo.

"Tuna mikoa 31 na wilaya 169 ambayo ina mabaraza ya majadiliano. Mabaraza hayo huongozwa na wakuu wa mikoa na wilaya na hupaswa kufanya mijadala mara mbili kwa mwaka," amesema.

Hata hivyo, amesema idadi nyingi ya mabaraza hayo hayafanyi vikao kwa wakati kwa sababu ya ukosefu wa fedha za muda mwingine utashi wa kisiasa.

Chanzo: mwananchi.co.tz