Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPSC yatumia mapato ya ndani kujenga ghorofa mbili

7a953ecd02c18c8fb0876c9b3628d990 TPSC yatumia mapato ya ndani kujenga ghorofa mbili

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHUO cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kimepongezwa kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kujenga jengo la ghorofa mbili lililoanza kutumika kutoa mafunzo katika fani mbalimbali Kampasi ya Tabora.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika mara baada ya kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.

Mkuchika alisema hatua ya kutumia fedha za ndani kujenga jengo lenye ofisi na madarasa, inapaswa kuigwa na taasisi nyingine za umma ambazo zinaitegemea Serikali kuwapatia fedha kuboresha ofisi zao.

“Kitendo cha kutumia fedha za ndani kwa maendeleo ya taifa ni jambo zuri ambalo Rais amekuwa akisisitiza mara kwa mara, hivyo, ujenzi wa jengo hili linanipa ujasiri wa kuwaalika Viongozi wa Kitaifa kulizindua rasmi, huku kipaumbele kikiwa kwa Rais mwenyewe,” alifafanua Mkuchika.

Akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dk Emmanuel Shindika alisema jengo hilo limekamilika na kuanza kutumika kabla ya uzinduzi rasmi .

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo linalojumuisha maktaba, vyumba vya madarasa ya kompyuta, kumbi, madarasa ya kawaida na ofisi za watumishi ulianza Novemba 5, 2014 na kukamilika rasmi Machi 26, 2020.

Chanzo: habarileo.co.tz