Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPHPA wafika Mbozi kunusuru mashamba ya wakulima

Wadudu Mashambani (600 X 154) TPHPA wafika Mbozi kunusuru mashamba ya wakulima

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesikia kilio cha wakulima wa mazao ya chakula na biashara katika kijiji cha ikomela kata ya kilimampimbi Wilayani Mbozi Mkoani Songwe ya kuharibiwa mazao yao na mdudu aina ya funza ambaye amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu hali iliyosababisha wakulima hao kupata hasara na kukada tamam na klima kutokana na mdudu huyo.

Ikiwa ni siku chache tangu Wasafimedia kutangaza taarifa ya uharibifu wa mashamba ya wakulima katika kijiji cha IKomela kata ya Kilimampimbi serikali tayari imeingilia kati suala hilo kwa kuwaleta Mamlaka ya Afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania (TPHPA) kufika mashambani ili kunusuru changamoto hiyo.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania (TPHPA) nyanza za Juu Kusini Emmanuel Mausa amesema wakuja kutokana na kuona tatizo hilo katika Vyombo vya Habari ambapo wametembelea baadhi ya mashamba ya kuchukua sampuli ya mdudu huyo huku akiwaondoa shaka wakulima na kuahidi kuleta majibu kwa kipindi kifupi.

Afisa Kilimo Wilaya ya Mbozi George Nipwapwacha amesema kutokana na kilio hicho cha wakulima wa ikomela na vijiji Jirani wataendelea na uhakiki ili kutathimini maeneo yaliyoathiriwa zaidi ili kupata takwimu sahihi na kutoa elimu kwa wakulima.

Kufuatia ujio wa wataalamu hao katika kijiji hicho wakulima pamoja na wananchi wameishukuru serikali kwa kuona tatizo lao na kuleta wataalamu kwani wamepata adha hiyo kwa kipindi kirefu huku wakiomba kupatiwa majibu kwa haraka ili waendane na msimu ujao wa Kilimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live