Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPDC yaongeza umiliki WentWorth

Mafuta Na Gesi TPDC yaongeza umiliki WentWorth

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania, kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), imenunua asilimia 20 zingine za hisa kutoka kwa kampuni ya kigeni ya WentWorth na sasa inamiliki asilimia 40, wakati kampuni ya Maurel and Promo (E&P) ikiwa na umiliki wa asilimia 60.

Gharama ya ununuzi wa hisa hizo imefikia Dola za Marekani milioni 23.6, sawa na Sh bilioni 60, ambayo yote ni mapato ya ndani ya TPDC.

Meneja wa Kampuni ya Maurel na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC wamesaini mikataba miwili muhimu, ikiwa ni pamoja na mauziano ya hisa za WentWorth na Mkataba wa Uendeshaji wa Kitalu cha Mnazibay.

Umiliki huu mpya wa hisa unapanua uwezo wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya shughuli za kampuni, na pia inatoa nafasi ya kura ya turufu katika majadiliano. Hii inaashiria hatua kubwa katika kuimarisha ushiriki wa ndani katika sekta muhimu ya gesi na mafuta.

TPDC sasa inapata fursa ya kupeleka wafanyakazi na kushiriki kikamilifu katika uendeshaji na uendelezaji wa vitalu vya mafuta na gesi. Kwa kuongeza, kuanzia mwaka huu, TPDC imepanga kuchimba visima viwili na kusimika mashine za mgandamizo ili kuboresha uzalishaji wa gesi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live