Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPDC yaomba kupunguziwa mzigo wa Deni la Serikali

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba ameiomba  serikali iwafutie malimbikizo ya deni lake katika vitabu vya fedha vya shirika hilo.

Kwa mujibu wa TPDC, Serikali imekuwa ikikopa na kulipa mikopo yote ya uwekeshaji katika shirika hilo na kisha kuorodhesha katika vitabu hivyo, TPDC ikitakiwa kurejesha fedha hizo kwa serikali.

Mkopo katika vitabu hivyo ni pamoja na dola 1.2 billioni za Mradi wa ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, ilizokopa kutoka benki ya Exim ya China.

 

Mhandisi Musomba ametoa kauli hiyo leo Mei 31,2019 jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.

"T unaomba mlitazame hilo kama Serikali ili kusaidia shirika liweze kuongeza mapato yake, "amesema Mhandisi Musomba.

Pia Soma

Kwa upande wa Godwin Kailembo, Kaimu Meneja wa Fedha na Utawala wa  shirika hilo amesema endapo serikali itawaondolea mkopo huo itasaidia shirika kuongeza mtaji wake  kifedha.

“Mkopo huo ukiondolewa faida ya shirika itaongezeka kutoka Sh9.57 bilioni hadi kufikia Sh131.2 bilioni kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2019.

“Kwa mwaka 2023 ,faida itafikia Sh159 bilioni ikilinganishwa na Sh59.62 bilioni ambayo itapatikana endapo serikali haitatufutia mikopo yake katika vitabu vya fedha," amesema Kailembo.

Akijibu suala hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji),  Angellah Kairuki ameahidi kuwasilisha ombi hilo serikalini.

Chanzo: mwananchi.co.tz