Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPDC yaishi agizo la Dk Biteko

Tanzania Itaenzi Umoja Wa Bara La Afrika   Biteko.png TPDC yaishi agizo la Dk Biteko

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtwara. Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC), limesaini hati ya makibaliano (MOU) baina yake na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Jeshi la Polisi Tanzania na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kwaajili ya ujenzi wa miradi mitatu katika Kata ya Msimbati.

Hafla hiyo imefanyika leo Ijumaa Novemba 24, 2023 katika Kijiji cha Msimbati mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame amesema miradi hiyo inatekelezwa kwa pamoja kwa kuwa ni maelekezo ya Naibu Waziri Mkuu.

“Sio mara yetu ya kwanza tumeshachangia miradi mingi ya zaidi ya Sh900 milioni kwaajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ambapo kupitia ziara ya Naibu Waziri Mkuu tumejifunza kuwatembelea wananchi na kuwa nao karibu,” amesema“

Kuanzia sasa tutakuwa na maofisa maendeleo ya jamii na mahusiano ya jamii ambao watakuwa hapa hapa kuanzia mwezi wa 12; kazi itaanza ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

”Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda amesema miradi itajengwa ndani ya siku 90 ambapo hadi kufikia April, 2024 tutakuwa tunakabidhi wananchi.“

Katika Zahanati yetu tutakuwa na majengo sita ya mama na mtoto, upasuaji, wangojwa wa nje, jengo la kutunzia dawa, maabala na nyumba ya watumishi wa afya ili kutoa huduma za ukakika kwa wananchi.

Lakini pia taa zitawekwa katika vijiji vya Madimba, Mngoji na Msimbati ili biashara ziweze kufanywa hata usiku,

” amesema Munkundakwa upande wake, Farida Mohamed Mkazi wa Kijjii cha Mtandi kata ya Msimbati amesema wamekuwa wakipata wakati mgumu kupata vipimo na matibabu katika zahanati ya Madimba hivyo kujengewa kwa kituo cha afya kutaboresha utolewaji wa huduma za afya katika kijiji hicho.“

Sisi tulikuwa tunasubiria kwa muda mrefu tena kwa hamu sana kupata kituo cha afya kikubwa kwakuwa zahanati yetu haina vipimo tulikuwa tunakwenda mjini hata UTI tulikuwa tunaenda kupima mjini ujenzi wa kituo cha afya hapa kwetu ni maendeleo makubwa

” amesema MohamedHemed Hassan, mkazi wa Kijiji cha Msimbati amesema huduma nyingi za afya walilazimika kwenda Mtwara mjini hali ambayo ilikuwa ikiongeza gharama za matibabu kwa mgonjwa.

“Unajua adha ilikuwa kubwa yaani ukipata tatizo kubwa ilikuwa ni changamoto wahudumu wachache hakuna ambulance wakati mwingine tunateseka kupata usafiri mfano mimi nilipoumia nilipelekwa pale lakini walishindwa kunihudumia nikapewa kikaratasi ikabidi niondoke kwenda Ligula angalia umbali uliopo lakini ingekuwepo zahanati ingesaidia” amesema Hassan

Chanzo: www.tanzaniaweb.live