Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPDC yafanya maboresho Mnazibay kuongeza uzalishaji

Tpdc Pic TPDC yafanya maboresho Mnazibay kuongeza uzalishaji

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limefanya maboresho katika kisima namba moja cha Mnazibay ili kuongeza uzalishaji wa gesi hiyo kutoka futi za ujazo mil10 zilizokuwa zinazalishwa awali na kuongeza futi za ujazo mil7.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kisima cha Mnazibay Msimbati mtwara wakati matengenezo hayo yakiendelea katika kisima hicho ambacho kipo ndani ya bahari Meneja wa Uendelezaji na Uzalisha wa Gesi TPDC, Mhandisi Felix Nanguka amesema kuwa zoezi hilo ni kwa ajili ya maandalizi ya ukarabati wa visima vyote vya gesi ili kuweza kuongeza uzalishaji wa gesi ambayo kwa sasa matumizi yake yameongezeka.

“Tunavyo visima vitano ambavyo vitafanyiwa maboresho na sasa tumeanza na kisima namba moja ambacho ni cha kwanza kisima hiki kinazalisha gesi futi za ujazo mil10 kwa siku ambacho tunaongeza uzalishaji futi mil 7 hivyo zitakuwa mil17,” amesema.

“Tunampango wa kuendeleza vitaru vingine kwaajiliya kuongeza uzalishaji wa gesi ambapo matumizi yameongezeka kwa kiwango kikubwa hivyo uboreshaji huu unaenda kuongeza kiasi cha gesi ambacho kinaenda kutumika katika uzalishaji wa umeme na matumizi majumbani,” amesema.

“Kwa mkoa wa Mtwara hiki pekee ndio kiko baharini lakini kwa songosongo tunavyo vinne ambavyo viko baharini kuanzia 2010-14 tulichimba visima zaidi ya 33 baharini kitalu no 1, 2, 4 ambapo visima hivyo vitaendelezwa kwaajiliya kiwanda cha LNG kinachotarajia kujengwa mkoani Lindi mpaka sasa tuna visima 104 nchini,” amesema Mhandisi Nanguka.

Mhandisi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Lessa Saimon amesema kuwa ukarabati utaongeza uzalishaji ambapo gesi hiyo itatumwa katika kiwanda cha kuchakata gesi madimba kwa ajili ya uzalishaji wa umeme nchini.

Nae Francis Mpokera Afisa Mahusiano wa TPDC amesema kuwa kazi ya shirika hilo ni kuhakikisha kuwa nishati inapatikana na kuendelezwa kwakuwa ndiyo gurudumu la taifa.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa Uzalishaji Maurel & Prom, Hussein Chitemo amesema kuwa oparesheni inayooendelea inafanywa katika kisima cha Mnazibay namba moja.

“Maboresho hayo yanatuwezesha sisi kuingiza vifaa maalumu kwenye visima ambacho kitasaidia kuongeza baada ya hili zoezi tunatarajia kuongeza futi za ujazo uniti 7 ambazo zitachangia uzalishaji wa gesi inayotumika kuzalishia umeme na matumizi mengine ambapo maboresho hayo yataachukua siku nne kukamilika,” amesema Chitemo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live