Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) limepanga kutekeleza miradi ya kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu na biashara kwa ajili ya jamii zilizohamishwa katika eneo la Likong'oko Manispaa ya Lindi kupisha mradi wa gesi asilia ya kusindika - LNG.
Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) limepanga kutekeleza miradi ya kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu na biashara kwa ajili ya jamii zilizohamishwa katika eneo la Likong'oko Manispaa ya Lindi kupisha mradi wa gesi asilia ya kusindika - LNG. Mkurungezi wa Kampuni ya Ushauri na Usimamizi wa Miradi ya RSK Tanzania, Jesper Johnson amesema lengo la Miradi hiyo (mradi wa kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu na biashara) ni kuhakikisha wanarudisha hali ya uchumi ya jamii iliyohamishwa kutoka eneo la mradi wa LNG.