Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPDC kuongeza uzalishaji gesi

Gesiii TPDC kuongeza uzalishaji gesi

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), limeanza kukarabati kisima namba moja cha kuzalisha gesi asilia Mnazi Bay, mkoani Mtwara, ili kuongeza tija katika uzalishaji wa umeme nchini.

Kisima hicho ambacho kwa sasa kinazalisha gesi futi za ujazo milioni 10 kwa siku. kiligundulika mwanzoni mwa mwaka 1982 na kuanza kuzalisha gesi mwaka 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari katika la kisima hicho, ambacho kipo eneo la baharini Mnazi Bay, Meneja wa Uendelezaji na Uzalishaji wa Gesi TPDC, Mhandisi Felix Nanguka suala hilo linafanyika ili kuongeza uzalishaji kutoka futi za ujazo milioni 10 kwa siku mpaka milioni 17 kwa siku.

"Kisima hiki kwa sasa kina uwezo wa kuzalisha gesi futi za ujazo milioni 10 kwa siku, ambapo tunatarajia kuongeza futi za ujazo milioni 7 na kufikia futi za ujazo milioni 17 kwa siku," amesema.

Amesema suala la ukarabati wa kisima hicho inatokana na ongezeko la matumizi ya gesi nchini na kuwalazimu shirika hilo kufanya ukarabati katika kisima hicho kuongeza uzalisha

Chanzo: www.tanzaniaweb.live