Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPC yaongeza uzalishaji wa sukari

Sukari Zanzibar TPC yaongeza uzalishaji wa sukari

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

iwanda cha sukari Moshi (TPC) kimeongeza uzalishaji wake wa sukari kutoka tani 108,000 zilizokuwa zikizalishwa kwa mwaka hadi kufikia tani 108,800 mwaka huu ikilinganishwa na uzalishaji wake wa msimu uliopita.

Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu na Utawala wa kiwanda hicho, Jafary Ally wakati wakufunga msimu wa uzalishaji wa sukari hadi hapo ifikapo Juni mwaka huu ambapo amesema licha ya kufunga msimu huo lakini sukari ipo ya kutosha.

"Kiwanda hiki cha sukari kinazalisha tani za sukari 108,000 lakini mwaka huu tumezalisha tani 108,800 imekuwa ni rekodi nzuri ya uzalishaji wa sukari hapa nchini,"amesema

Aidha amesema kiwanda hicho kimeboresha uzalishaji wa sukari kutoka tani 36,000 zilizo kuwa zikizalishwa mwaka 2000 hadi kufikia tani 108,000 kwa mwaka huku miwa ikizalishwa kutoka tani 360,000 hadi kufikia tani milioni 1.1 kwa mwaka.

Amesema mwaka 2000 walikuwa wakichangia pato la Taifa Sh2 bilioni ambapo kwa sasa wanachangia zaidi ya Sh90 bilioni sehemu kubwa ikiwa ni kwenye kodi huku wakitoa gawio kwa serikali la Sh15 bilioni kwa mwaka.

"Kwa miaka mitano iliyopita tangu mwaka 2017 kiwanda cha Sukari cha TPC hakijawahi kupandisha bei kubwa ya sukari,kuanzia mwaka 2017 hadi leo mwaka 2022 kiwango cha sukari kilichoongezeka kwenye bei ni Sh100 tuu kwa kilo ,"

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai alikipongeza kiwanda hicho kwa kuchangia maendeleo katika jamii inayowazunguka na kuhakikisha wanasaidia kuboresha miundo mbinu ya shule na barabara.

"Mkoa wa Kilimanjaro tunajivunia uwepo wenu hapa ,sisi kama serikali tutahakikisha tunawalinda na kuwawekea mazingira mazuri ya uzalishaji ili uzalishaji uendelee kuwa mkubwa zaidi,mmekuwa wawekezaji wazuri katika nchi hii,"amesema Kagaigai

Chanzo: www.tanzaniaweb.live