Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPB, NIC kuboresha huduma zao pamoja

Fd4cad1273402be72bb84ad4b40fe3dc TPB, NIC kuboresha huduma zao pamoja

Sun, 7 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imeingia ushirikiano na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa ajili ya kuboresha huduma za taasisi hizo, zikihusisha upatikanaji wa bima katika matawi yote ya TPB.

Viongozi wakuu wa taasisi hizo walisema hatua hiyo ina faida kubwa kwa TPB na NIC na zaidi itawarahisishia wananchi kupata huduma. Walisema hayo wakati wa hafla ya kutambulisha ushirikiano huo.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi alisema kuwa hiyo ni hatua nzuri itakayozisaidia taasisi hizo za Serikali kuongeza ufanisi wake wa kiutendaji na kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za bima kote nchini.

“Kimsingi idadi ya watumiaji wa huduma za bima nchini bado ni ndogo na kwa kuwa lengo la NIC ni kuhakikisha zaidi ya asilimia ya wananchi nchini wanapata huduma hiyo, ushirikiano wake ni TPB itasaidia katika kulifikia lengo hilo,” alisema Moshingi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo aliishukuru NIC kwa kufanya kujenga mashirikiano hayo ambayo aliahidi kuwa wao kama TPB watayaboresha ili yawapatie tija na kwa wananchi pia.

Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dk Elirehema Doriye aliishukuru TPB kwa kukubali kuingia ushirikiano huo. Alisema hatua hiyo inakwenda kuongeza ufanisi katika sekta ya bima.

Alisema hiyo ni kutokana na dhamira ya taasisi hiyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi, baada ya kusogeza huduma karibu na maeneo walipo, tofauti na zamani ambapo huduma za bima zilikuwa zinatolewa katika matawi ya NIC pekee.

Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika matawi ya TPB na NIC ili wapate huduma za bima.

Mkurugenzi huyo alisema taasisi hiyo 'imerudi upya' katika kutoa huduma bora kwa wananchi, ambapo hivi karibuni ilizindua huduma za BimaFlex, ambayo ni maalumu kwa wamiliki wa magari.

Chanzo: www.habarileo.co.tz