Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yatoa mchongo mzima usafirishaji makaa ya mawe Ulaya

Makaa Ya Mawe Mtwara TPA yatoa mchongo mzima usafirishaji makaa ya mawe Ulaya

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imewashauri wafanyabiashara kuungana mkono ili kuchangamkia fursa za kusafirisha makaa ya mawe nje ya nchi.

Kaimu meneja wa bandari ya Mtwara, Bw Nobert Kalembwe alitoa wito huo baada ya kampuni nne kufanikiwa kuuza tani 57,300 za makaa ya mawe kwa kampuni inayofanya usafirishaji wa bidhaa hiyo kwenda Poland . "Ikiwa mmoja ana shehena ndogo na mwinginepia anayo ndogo , ukiizikusanya unapata shehena ya kutosha kusafirishwa," Bw Kalembwe alisema. Kampuni hizo nne ni pamoja na Milco, Sebdo, Beco na Tancoal, ambazo ziliuzwa kwa Amex ambayo ilisafirisha makaa ya mawe nchini Poland.

Afisa mkuu mtendaji wa Amex Group Filip Celadnic alisema ni mafanikio makubwa kwao kusafirisha makaa ya mawe katika soko la Ulaya na kuongeza kuwaTanzania itakuwa nchi pekee duniani ambayo inaweza kusambaza makaa ya mawe Ulaya.

"Huu umekuwa uwekezaji mkubwa uliofikiwa kupitia juhudi za watu wengi, ikiwa ni pamoja na serikali na mamlaka zake," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live