Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yatenganisha eneo la Bandari Bagamoyo

Bandari Bagamoyo Kutenganishwa TPA yatenganisha eneo la Bandari Bagamoyo

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imeamua kutenganisha utekelezaji wa mradi huo na mradi wa eneo maalumu la kiuchumi Bagamoyo.

Awali, ilielezwa ujenzi wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo utahusisha pia ujenzi wa mradi wa eneo maalumu la kiuchumi.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Januari 9, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa alipozungumza na waandishi wa habari.

"Tunaanzia na gati mbili ndefu na hizo zitajengwa na sisi TPA, baadaye zinazofuata na tupo tayari kupokea mwekezaji kutoka sekta binafsi atakayejenga kwa kushirikiana na serikali," amesema.

Amesema awali mpango ulikuwa ujenzi wa mradi huo uhusishe na ujenzi wa eneo maalumu la uchumi lakini wameamua kutekeleza miradi hiyo kwa nyakati tofauti.

"Tumeona haja ya kuharakisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kutokana na hali iliyopo, kwamba baadhi ya meli haziwezi kuhudumiwa na Bandari ya Dar es Salaam kutokana na magati kuwa mdogo," amesema.

Hata hivyo, Mbossa amesema wanatarajia mradi huo kukamilika mwaka 2028 na kwa sasa mchakato wa kumpata mzabuni unaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live