Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yatenga Bil 429.1 bandari ya Tanga

TPA Msemaji TPA yatenga Bil 429.1 bandari ya Tanga

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimsimizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetenga fedha jumla ya bil. 429.1 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa na wa kimkakati wa Bandari ya Tanga, ambapo unatekelezwa katika awamu mbili,huku mradi huo unatarajiwa kukamilika 28 Novemba2022 ambapo umekamilika kwa 61%

Akizungumza Msemaji wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi amesema kuwa mradi wa awamu ya kwanza ulihusisha uchimbaji wa kina cha maji kwenye mlango kuingilia meli kutoka mita 3 hadi 13 kwa gharama ya sh.bil 172.3 ambapo awamu ya pili ukihusisha ujenzi wa gati mbili unaogharimu bil.256.8

Aidha kwa mwaka wa fedha 2021/22 TPA wameweza kuvuka lengo kwa kuhudumia jumla ya tani 867,000 hata hivyo ni matokeo ya awali mara baada ya uwekezaji mkubwa wa uboreshaji wa Bandari ya Tanga kuanza kufanyika tokea 2019

"TPA agisti 3,2019 iliingia mkataba wa miezi 12 Kampuni ya kichina Harbaour Engineering company (CHEC)Limited ambaoo Mhandisi wa mradi huu ni kampuni ya NIRAS kutika Dermack ikishirikiana na Kampuni ya kizawa ijukukanayi kwa jina la ANOVA".Alisema

Milanzi alisema kuwa hadi kufikia mwezi agosti 2022 ,tayari Mkandarasi ameshakabidhi kipande ha urefu wa mita 200 ambapo hatua hiyo inaiwezesha Bandari ya Tanga kuanza kupokea meli na kuhudumia meli getini zisizozidi mita 200kama inavyofanyika katika bandari ya Dar es salaam.

Amesemaa kuwa Matarajio ya Serikali na Mamlaka ya Bandari kutokana na mradi wa maboresho hayo yenye uwekezaji mkubwa uliofanywa katika mradi, utakapokamilika utakuwa na faida nyingi ikiwemo kuongezekankwa shehena 750,000 za sasa hadi kufikia tani 3,000,000 kupitia bandari ya Tanga,shehena ya makasha kutoka TEUS 12,000za sasa hadi TEUS 30,000,

"Tunamshukuru Mhe Rais kwa kutekeleza b mradi huu wa kimkakati bila matatizo yeyote kwani amehakikisha unatekelezwa kama ulivyopangwa."alisema Milanzi

Rose Tandiko ni Afisa masoko Bandari ya Tanga Akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari Afisa habari wa TPA,alisema kuwa Bandari hiyo haijawahi kuwa na urasimu kwani kutokana na mfumo wateja wnaaweza kutoa mizigo ndani ya masaa 24 iwapo wamekalilisha nyaraka zote muhimu za utoaji wa mizigo,kwani uchelewaji wa. Utoaji mizigo unaweza kuchangiwa na mteja mwenyewe"

"Wadau wote wanaohisika kutoa mizigo katika bandari ya Tanga wapo katika eneo moja kwa maana hiyo mdau atakapokamilisha taratibu zote mzigo unaatolewa kwa wakati"alisema Tandiko

Tandiko amesema kuwa kukamilika kwa bandari hiyo kutafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa mikoa ya kaskazini mwa Tanzania pamoja na nchi jirani,sambamba na kutoa fursa za ajira kw awanachi m,pia kupungua gharama za uendeshaji wa Bandari kutokana na mtindo wa kuhudumia meli ikiwa nangani kwa kitumia matishari

Hamis Kipalo ni Mhandishi wa Bandari ya Tanga ameainisha mitambo iliyonunuliwa ili kukamilisha marekebisho hayo kuwa ni pamoja na Forklif mbili tani 5,front loader forklift moja ya tani 50,empty container Handlermoja ya tani 6,terminal Tractor( TT)mbili ,Grab moja ya Tani 10 na uweO wa kubeba mzigo tani 15,Rubber Tyred Granty RTG moja ya tani 40,Spreader nne mbili za futi 40 na mbili za futi 20,Bale Clamp Forklift mbili za tani3,Gottwald mbili za tani 100 pamoja na Forklift moja ya tani 16.

Aidha Bandari ya Tanga ni moja ya Bandari kongwe uliyojengwa katika PWANI ya Afrika ya Mashariki na kuanza kufanya kaI nwaka 1891 wakati wa kioindi cha utawala wa ukoloni wa Kijerumani Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live