Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yataka ushirikiano maboresho ya bandari

Bandari Tanga Tangaaa TPA yataka ushirikiano maboresho ya bandari

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ushirikiano baina ya taasisi za Umma na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) unahitajika ili kufanikisha azma ya Serikali ya kufanya maboresho makubwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA Balozi Ernest Mangu mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kutembelea Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujionea maboresho yaliyofanyika.

"Tumeeleza namna ambavyo tunahitaji kuendelea kupanua Bandari ya Dar es Salaam zikiwemo bandari kavu, na taasisi za Serikali zinatakiwa zitusadie kuwezesha upanuzi huo na kukidhi mahitaji ya wateja wengi zaidi,"Amesema Balozi Mangu.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa Bandari ya Tanga kumesaidia kupokea baadhi ya meli ambazo zilitakiwa kushusha mzigo katika Bandari ya Dar es Salaam na bandari ya Mombasa nchini Kenya ambapo kwa sasa zinakwenda Tanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa PIC Deus Sangu amesema kamati yake ina jukumu la kuangalia uwekezaji wa mitaji ya umma ikiwemo maboresho katika bandari ya Dar es Salaam ambayo uwekezaji wake umekuwa na tija katika ukusanyaji mapato kutoka zaidi ya shilingi Bilioni 800 hadi kufikia shilingi Trilioni 1.4 kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live