Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yashauriwa kurasimisha bandari bubu

Bandari Bubu TPA yashauriwa kurasimisha bandari bubu

Tue, 8 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Menejimenti ya Bodi ya Shirika la Wakala wa Meli nchini (TASAC) imeishauri Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kuharakisha urasimishaji wa bandari bubu ili kuokoa mapato yanayopotea.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Kapteni Musa Mandia wakati wa ziara yake ya kutembelea uboreshwaji wa miundombinu ya Bandari ya Tanga.

"Iwapo bandari bubu zitarasimishwa zitaweza kudhibiti upotevu wa mapato ambao unatokea katika maeneo hayo pamoja na kudhibiti wafanyabiashara wanaokwepa kodi, amesema.

Mwenyekiti huyo amezungumzia namna upanuzi wa kina cha bandari hiyo utakavyoongeza ufanisi wa utendaji kazi pamoja na usalama wa bandari hiyo.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Masoud Mrisha amesema kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu katika bandari hiyo kutawezesha kuongeza uwezo wa bandari hiyo kutoka tani 700,000 hadi 3,000,000.

Kwa upande wake mkandarasi anayejenga miundombinu ya gati katika bandari hiyo amesema ujenzi wa awamu ya kwanza umekamilika kwa zaidi ya asilimia 35 ambapo wanatarajia kukabidhi kazi mwezi Mei mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live