Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yapongezwa usimamizi maboresho ya Bandari Dar

TPA Yapongezwa Usimamizi Maboresho Ya Bandari Dar TPA yapongezwa usimamizi maboresho ya Bandari Dar

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania - TPA kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam.

Pongezi hizo za Kamati zimetolewa tarehe 15 Novemba,2023 na Mwenyekiti wake Mhe. Selemani Kakoso ( Mb) baada ya kumaliza ziara yao wakiongozana na Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo wametembelea na kukagua utendaji na miradi ya maboresho ya miondombinu katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mhe. Kakoso amesisitiza umuhimu wa TPA kuongeza ufanisi zaidi katika usimamizi vema wa miradi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam iliyotekelezwa ili kuongeza tija, kukusanya mapato zaidi na kuvutia Wateja na Wadau wengi wa bandari hiyo.

Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ( Mb) amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu mingine inayounganisha shughuli za bandari ikiwemo Reli ili kuongeza ufanisi wa kuhudumia Shehena Bandarini.

Mapema akitoa taarifa ya maboresho na utendaji kazi wa Bandari ya DSM, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa, amesema kumekuwa na ongezeko la idadi ya meli za mizigo zinazohudumiwa Katika Bandari hiyo, kutoka Meli 1,511 kwa mwaka 2020/2021 hadi meli kufikia Meli 1,743 kwa mwaka 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live