Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yapewa maagizo bandari Bukoba

04cd038dd49940f5bd6c910b297179b1 TPA yapewa maagizo bandari Bukoba

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ameitaka Mamlaka ya Usimamizi Bandari nchini (TPA), kitengo cha ununuzi kukamilisha haraka, mchakato wa kupata mkandarasi wa kutengeneza miundombinu Bandari ya Bukoba na Kemondo.

Amesema hatua hiyo itawezesha meli ya Mv Mwanza inayotarajia kufanya kazi Afrika Mashariki kutia nanga kwenye bandari hizo.

Alisema kutakuwa na upanuzi wa gati katika bandari ya Kemondo, ujenzi wa gati mpya katika bandari ya Bukoba na kuongeza kina cha maji bandari ya Bukoba, mradi unaotarajia kugharimu Sh. Bilioni 23.

Alisema mchakato unapaswa kufanywa haraka na TPA, kwani ujenzi wa meli mpya ambayo itaanya kazi kati ya bandari ya Mwanza na Kemondo na hatimaye bandari za Kenya na Uganda unatarajia kukamilika Septemba mwaka huu, lakini kama mchakato wa upanuzi bandari hautakamilika, meli hiyo haitaweza kuanza safari zake.

Alisema bandari zikisimamiwa kwa ukamilifu na umakini mkubwa, zinaweza kuchangia nusu ya bajeti ya nchi kila mwaka, lakini kufikia hatu hiyo kunahitaji maboresho ya miundombinu na usimamizi mzuri wa bandari zilizopo nchini.

Kwa mujibu wa Ofisa Mfawidhi wa bandari ya Bukoba, Denis Mapunda, bandari hiyo kwa sasa inawezesha meli tatu kutia nanga kwa wakati mmoja, kutoa huduma za kubeba mizigo na abiria.

Alisema baada ya huduma za meli kurejea wanafanya jitihada za kuzungumza na wateja wakubwa kutoka Uganda, ambao wamekuwa wakifirisha bidhaa kwa magari kuja Bukoba na Mwanza, kuhakikisha wanatumia meli kusafirisha mizigo yao, jambo ambalo anasema limefanikiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live