Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yapata Tril. 1.1/- kuboresha ufanisi wa bandari

DYD7z GXkAA6AF1 TPA yapata Tril. 1.1/- kuboresha ufanisi wa bandari

Tue, 1 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Kimataifa ya Uchukuzi na ‘Logistic’ ya DPW ya Umoja wa Falme za Kiarabu itatumia Dola za Kimarekani milioni 500 (sawa Sh. 1,161,086,870,197) katika miradi mbalimbali iliyolenga kuboresha ufanisi katika bandari zinazomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Taarifa iliyotolea na TPA jana, ilisema makubaliano ya kupatikana kwa fedha hizo yalitiwa saini katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dubai (Dubai Export 2020) kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA, Eric Hamissi na Mtendaji Mkuu wa DPW, Sultan Ahmed Bin Sulayem.

Ilisema makubaliano ya ushirikiano (MoU) yaliyofikiwa ni sehemu ya matukio muhimu wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan, nchini Dubai aliyehudhuria Siku ya Tanzania katika maonyesho hayo juzi.

Fedha zilizopatikana zitatumika kuendeleza Bandari za Tanzania kwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA, mafunzo kwa watumishi na uendelezaji wa miundombinu ya kibandari katika Bandari za Mwambao wa Bahari na Maziwa.

Fedha hizo pia zitatumika kwa ajili ya kuiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuongeza ushindani wake katika viwango vya kimataifa vya ubora na ufanisi wa huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live