Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA yachukua hatua kudhibiti ubadhirifu

F8fb86b5f2cb1909555cdeb02bc9b6bf.png TPA yachukua hatua kudhibiti ubadhirifu

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeanza kuchukua hatua kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za mamlaka hiyo.

TPA imetangaza hivyo zikiwa zimepita siku 24 tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, awasimamishe kazi Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Nuru Mhando na Meneja wa Matumizi ya Fedha wa TPA, Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazowakabili.

Waziri Mkuu alifanya uamuzi huo Desemba 27 mwaka jana jijini Dar es Salaam katika kikao cna Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya mamlaka hiyo, Menejimenti ya TPA, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru na Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI) kilichofanyika katika ofisi za TPA.

Akijibu maswali ya Jukwaa la Wahariri na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusidedit Kakoko, alisema moja ya hatua zilizochukuliwa baada ya waziri Mkuu kutoa agizo la uchunguzi kufanywa kwa watendaji hao na wengine, ni pamoja na wao kuchunguza na kubaini wafanyakazi 33 walihusika kwenye sakata hilo.

“Sisi ndio tuliona kuna mwenendo unaotia shaka wa matumuzi ya fedha za TPA,tukamuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), afanya ukaguzi wa mahesabu hayo na sisi tumejiridhisha watumishi wetu 33 walihusika na 17, kati yao ajira zao zimekoma’’alisema Kakoko.

Kakoko alisema maagizo ya Waziri Mkuu ni sahihi na wao wanataka sakata hilo liendelee kuchunguzwa hadi mwisho ili kama kutabainika wasiohusika, warudishwe kazini na wale wanaohusika sheria ifuatwe mkondo.

Chanzo: habarileo.co.tz