Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA wapewa maagizo ujio New Mv Mwanza

F9d58d2cf8b3a018ff77359b7d0ef7cc TPA wapewa maagizo ujio New Mv Mwanza

Thu, 17 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ameitaka Mamlaka ya Usimamizi Bandari (TPA) Mkoa wa Mwanza kuhakikisha inajenga gati mpya, ili kutumika kuipokea meli ya New Mv Mwanza inayotarajiwa kukamilika ujenzi wake Septemba mwaka huu.

Mwakitebe alisema hayo leo wakati wa ziara yake katika bandari ya Mwanza North na Mwanza South.

‘’Ni wakati sasa TPA Mwanza kuanza mapema kutengeneza gati, ambapo meli mpya ikikamilika itakuwa inaegesha kabla ya kupakia na kuondoka,’’ alisema Mwakibete.

Ameiagiza TPA na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), kuhakikisha zinatafuta masoko mengi zaidi, ili kuweza kuwafikia wateja wao.

Alisema meli ya Mv Umoja itakapokamilika matengenezo yake pamoja na kukamilika kwa mradi wa Reli ya Kisasa ya (SGR), itasaidia sana kupeleka mizigo nchini Uganda na Kenya.

‘’Kwa sasa mizigo tunayopeleka Uganda ni asilimia 2 na mategemeo ya wizara yetu ni kuona tunapeleka mizigo angalau asilimia 40,’’ alisema Mwakibete.

Naye Kaimu Meneja Mamlaka ya Bandari ya Ziwa Victoria, Vicent Stephano, alisema mamlaka yao imejipanga kuhakikisha inaboresha gati katika bandari za Mwanza Kusini, Bukoba na Kemondo kwa kuhakikisha inajenga gati kwenye maeneo hayo yenye urefu wa mita 100.

Alisema meli ya New Mv Mwanza, itakuwa na urefu meta 92 na itakuwa inapita katika njia za Kemondo, Mwanza Kusini, Bukoba pamoja na kwenda nchi za Kenya na Uganda.

Alisema wamejipanga kuipokea meli mpya na wana imani kubwa, italeta maendeleo kwa kuongeza mapato.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live