Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA: tunafanyia kazi changamoto zilizopo bandarini

Wabunge EALA Wahadharisha Ubaguzi Uwekezaji Wa Bandari TPA: tunafanyia kazi changamoto zilizopo bandarini

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho, amesema wanafanya kazi kwa Saa 24 ikiwemo wikiendi kukabiliana na changamoto ya Mizigo kuchelewa kutoka ili kuhakikisha Meli zilizopo kwenye foleni zinatoka

Tamko hilo limetolewa siku chache tangu Mdau kudai kuna Mazingira ya Urasimu katika Bandari hiyo hali inayosababisha Mizigo kuchelewa kutoka, badala ya wiki moja au mbili wanalazimika kusubiri zaidi ya Miezi miwili

Mrisho anasema “Watanzania hasa wateja wetu wawe wanatuelewa kuwa kuanzia Oktoba na mwanzo wa Mwaka kuna ongezeko kubwa la Meli, ndio maana tuna ‘shift’ tatu ndani ya Saa 24 na tunaomba Meli ziendelee kuja kwa kuwa ndio Uchumi wa Taifa hili.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live